Friday, December 12, 2014

MKUTANO WA KUFUNGA KAMPENI ZA SERIKALI ZA MTAA WAFANA JIMBO LA ILALA



 Wapenzi na Wanachama wa CCM wakijumuika pamoja wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa Jimbo la Ilala.
 Wasanii wa bendi ya Twanga Pepeta wakitumbuiza wakati wa kufunga kampeni za CCM jimbo la Ilala ,mkutano uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.
 Wanachama wakionyesha mabango ya wagombea wao.
 Mbunge wa Jimbo la Ilala  Mhe. Mussa Azzan Zungu (CCM)akihutubia wakati wa kufunga mkutano wa kampeni za serikali za mitaa Jimbo la Ilala ambapo aliitaka serikali kutambua Ilala ni sehemu ya biashara hivyo hakuna budi kuwaacha watu wafanye biashara.
 Kila wakati wanachama walionekana kushangilia hotuba zao.
 Wanachama wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wao.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida akisalimia wananchi wa Jimbo la Ilala wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa jimbo la ilala zilizofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Jimbo la Ilala wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za serikali za mitaa Jimbo la Ilala uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.
 Mbunge wa Jimbo la Ilala ni: Mhe. Mussa Azzan Zungu (CCM)akizungumza na mtoto mmoja aliyekuwa kwenye eneo la mkutano.
 Gungu Mohamed Tambaza mgombea wanafasi ya Uenyekiti wa Serikali za Mitaa Mtambani B akiomba kura kwa niaba ya wagombea wenzake wa jimbo la Ilala wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa  kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.
Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Abilahi Mihewa akisalimia wananchi wa Jimbo la Ilala waliojitokeza kwa wingi wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa 

 Kada wa CCM Haji Manara  akiwasalimu wakazi wa Jimbo la Ilala wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru ambapo aliwaambia wananchi hao ilala ni sehemu salama sana kwa CCM na historia ya CCM imeanzia Ilala.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Kada wa CCM Haji Manara kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CCM serikali za mitaa uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.
 Kada wa CCM Haji Manara akicheza na wapenzi wa wanachama wa CCM wakati wa kufunga kampeni za CCM jimbo la ilala kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.
 Ilala ni sehemu salama kwa CCM.
 Kila mtu alichukua tukio apendavyo
 Haji Kube Katibu wa Jimbo la Ilala akiongoza taratibu za mkutano wa ufungaji kampeni katika jimbo hilo uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.

No comments:

Post a Comment