Tuesday, April 15, 2014

KINANA WILAYANI MLELE
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mama Mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipomtembelea nyumbani kwake Kibaoni wilaya ya Mlele,Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kujenga na kukiimarisha Chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kupanda ngazi za tanki la maji linalojengwa kibaoni ikiwa moja ya miradi ya kusogeza huduma za maji kwa wananchi kijiji cha Kibaoni.

 Moja ya kibanda cha kuhifadhia mizinga ya nyuki kwenye shamaba la Waziri Mkuu Mizengo Pinda kijijini kwake Kibaoni wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya namna ya kufuga nyuki kutoka kwa Msaidizi wa Waziri Mkuu Jimboni Ndugu Charles Kanyanda.
 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka shambani kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda baada ya kujionea namna Nyuki anavyofugwa shambani hapo.
Katibu Mkuu wa CCM wa Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya mradi wa mashine ya kukoboa Mpunga kwenye kijiji cha Mwamapuli wilaya ya Mlele alipotembelea kujionea utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi na kuwaambia wananchi hao wasikubali kuuza ardhi bila utaratibu unaoeleweka kwani kunaweza kuwaletea migogoro mikubwa hapo baadae.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kucheza Kwaya ya Kisukuma yenye ujumbe wa Usalama kutoka kikundi cha Isimba walipotumbuiza kwenye viwanja vya Majimoto wilaya ya Mlele mkoani Katavi.