Saturday, March 28, 2015

PICHA ZA KUWASILI KWA MUGABE


13 14Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akishuka kwenye Ndege wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro International Airport (KIA) tayari kwa kuufungua mkutano wa Vijana Viongozi wa Afrika na China (African- China Young Leaders Forum) unaofanyika kwenye hoteli ya Ngurudoto Mkoani Arusha kwa siku 4 ukijumuisha vijana kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na China, Mzee Robert Mugabe amepokelewa na Makamu wa Rais Mh. Dr. Gharib Bilal kulia na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi mbalimbali wa CCM na serikali mkoani Arusha.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-ARUSHA) 15Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa KIA mkoani Arusha. 17Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akiongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA. 18Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akiongozana na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Gharib Bilal. 20Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe na Mwenyeji wake Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal wakiangalia vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa mapokezi, kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 21Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati walipokuwa wakiangalia vikundi vya ngoma vikitoa burudani. 22Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe, Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto wakiangalia vikundi vya ngoma. 24Rais Mugabe na mwenyeji wake Mamaku wa Rais Dr. Gharib Bilal pamoja na viongozi wengine wakielekea kwenye chumba cha mapumziko kwenye uwanja wa Ndege wa KIA. 25Mwenyekiti wa Kamati ya Maandaliazi Mh. Steven Masele akizungumza na vyombo vyahabari kwenye uwanja wa KIA mara baada ya kuwasili kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.

KONGAMANO LA VIJANA