Vijana hawa wawili walikamatwa kwenye mkutano wa CCM wakigawa vipeperushi vya Chadema bila wasiwasi hata hivyo viongozi wa CCM waliokuwa kwenye mkutano huo wa kampeni uliofanyika kijiji cha Mkoko kata ya Msata tarehe 24 Machi 2014, waliwaambia tu wanachofanya ni uvunjaji wa utaratibu hivyo kuwaomba waondoke eneo la mkutano huo na kusubiri zamu ya mkutano kisha ndio wasambaze vipeperushi vyao.